Tuesday, June 21, 2016

BET KUMPA TUZO YA HESHIMA AKON

Waandaaji wa tuzo za BET wametangaza kumpatia Akon tuzo ya heshima ya Global Good kwenye tuzo zitakazofanyika Los Angeles, Juni 26 mwaka huu.

Baghdad

Waandaaji wa tuzo hizo za BET wameamua kumpatia tuzo hiyo ya heshima Akon kutokana na mchango wake anaoutoa wa kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika kutokana na mradi wake wa umeme wa jua ‘Akon Lighting Africa’ ulioanza kazi mwaka jana huku akipanga kusaidia zaidi ya watu milioni 600.

Akon anapewa tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika muziki kwani ni mmoja kati ya watu waliotoa mchango wao kutengeneza mziki wa marekani na dunia kwa ujumla.

Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka jana kwa watu wanaotoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika na mtu wa kwanza kupatiwa tuzo hiyo alikuwa ni Miss Tanzania 2001, Millen Magesse.



No comments:

Post a Comment