Msanii wa muziki wa Hip Hop, Joh Makini amesema wasanii wa muziki kumudu
gharaza za kushoot video zao nje ni dalili nzuri ya mafanikio ya muziki
wa Tanzania.
Papper huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa muziki wa bongo fleva kwa sasa unajivua magamba kama nyoka na kuacha makapi na kwenda na watu wanaojua muziki wa kweli.
“Imefika hatua saizi watu wengi wanaweza kumudu gharama za kufanya video nje ya nchi na kupiga video kali na wanatengeneza muziki mzuri,” alisema Joh Makini.
Hata hivyo rapper huyo amewataka wasanii wenzake kuboresha muziki wao ili pachage ya video na audio iende sawa.
“Hivyo basi package yote hiyo lazima iwe full kuanzia kwenye audio mpaka video, lakini muziki lazima uanze kwanza kuwa mzuri kwani saizi watu hawashangaa sana video sababu wanarudisha masikio yao kwenye muziki mzuri. Mwisho wa siku haya yote yanaanzia kwenye muziki yaani studio. Nachoweza kusema turudi kwenye muziki saizi hakuna ujanja ujanja tena,” alisema Joh.

No comments:
Post a Comment