Wednesday, July 20, 2016

KALA JEREMIAH AFICHUA MAAJABU YA MTOTO ALIYEMSHIRIKISHA KATIKA NGOMA YAKE MPYA "WANA NDOTO"

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah anaendelea na nyimbo zake za kiuwanaharakati ambapo anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Wana Ndoto’ aliomshirikisha binti mdogo.

ffff

Rapper huyo alisema wimbo huo unazungumzia maisha ya jamii pamoja na watoto wadogo ambao wanandozo za kufanya mambo fulani katika maisha yao.

Jumatano hii, Kala ameamua kuweka wazi uwezo na binti huyo ambaye amemshirikisha katika wimbo huo.
“Nimewahi kukutana na watoto wengi wenye vipaji lakini sijawahi kukutana na mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu kama huyu mtoto,” aliandika Kala kupitia instagram.

Aliongeza, “Anauwezo mkubwa sana wa kuimba na ana akili nyingi sana. Mungu kambariki sana. Ukitaka kuamini hayo subiri tarehe 26/7 /2016 siku ambayo ‪#‎wanandoto‬ inatoka. huyu ndiye kaimba kiitikio. wakati unaendelea kusubiri Wana Ndoto unaweza kwenda youtube na kuandika miriam chirwa utaona mambo yake. na utaamini ninachokisema,”

No comments:

Post a Comment