Wednesday, September 24, 2014

MENEJA WA DIAMOND, BABU TALE AZUNGUMZIA UJIO MPYA WA NGOMA ZA DIAMOND.

 http://naibuzz.com/wp-content/uploads/2014/07/dia11.jpg

Wakati wimbo wa MdogoMdogo ukiwa bado unasumbua kwenye media, Diamond Platinumz anatarajia kurusha mawe mengine mazito zaidi kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wake.

Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond amesema mkali huyo anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo na kwamba zote zimetayarishwa nje.
“Tusubirie kidogo, baada ya miezi miwili mitatu tutaongea kwa sababu kuna kazi zinakuja, Diamond anarelease ngoma mbili mfululizo na zote zimetoka nje. Lakini hatuwezi kueongea sasa hivi hadi muda ufike.” Babu Tale 
Inaonekana Diamond hataki kuacha gap, anakandamizia palepale azidi kwenda juu na kutwaa tuzo nyingi za kimataifa kama alivyofanya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment