Wednesday, September 24, 2014

 Justin Bieber aacha pombe, atanganza maisha mapya na Selena Gomez

Mwimbaji Justine Bieber ameamua kuyaanza maisha mapya kwa kuacha kutumia vilevi na vyakula visivyoshauriwa kiafya ili kuinusuru zaidi kazi yake ya muziki.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Justine Beiber amekua akijigamba mbele ya marafiki zake kuhusu maisha mapya ya afya bora.

"Bieber hanywi tena pombe na ameacha kula vyakula visivyoshauriwa kiafya pia. Alikua katika wakati mgumu katika miezi michache iliyopita na anatumaini hii itampa mwanzo mzuri." Kimeeleza chanzo icho.
Mwimbaji huyo amekua katika matatizo ya kisheria hivi karibuni, anaonekana kuyaanza maisha mapya katika uhusiano wake pia baaba ya kutangaza kua yuko tayari kua na familia na anataka kumuoa mpenzi wake Serena Gomez.

No comments:

Post a Comment