Wednesday, November 12, 2014

RAPPER GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA.

Rapper mahiri aliyewahi kutamba na ngoma kibao kama Mtoto wa kiume Geez Mabov afariki dunia usiku wa kuamkia jumatano mjini Iringa.

GEEZ MABOVU.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez alienda kwao Iringa wiki moja na nusu iliyopita ambapo alianza kuugua mfululizo.

Wasanii wenzake wameendelea kutuma salamu za rambi rambi huku wengine kuhairisha show zao ambazo walitakiwa kuzifanya ndani ya wiki hii na wengine kuhairisha kuachia ngoma zao mpya ambazo pia zilitakiwa kutoka wiki hii, Young killer ni mmoja kati ya rappers ambao wangetakiwa kuachia video ya ngoma yake mpya aliyofanya na Fid Q, ambayo ilitakiwa kutoka November 13.

Weusi nao wamehairisha show yao ya Mbeya ambayo ilitakiwa kufanyika kukwepa msiba wa Geez Mabov. Rest in peace Brother Geez.

No comments:

Post a Comment