Saturday, January 24, 2015

MABESTE KUMALIZA TOFAUTI ZAKE NA B-HITS

MABESTE.
Rapper kutoka Dole Entertainment, Mabeste, amesema kamaliza tofauti zake na management yake ya zamani ya B-hits, mgogoro ambao ulisababisha mabeste kujiondoa katika Record lebel hiyo, Mabeste ameyasema hayo jana akifanya mahojiano na clouds fm katika kipindi cha Xxl. vilevile amesema chuki siku zote azijengi bali hubomoa na kusababisha misundestand ambazo hazina umuhimu.


"Ili muziki usonge mbele kunahitajika maelewano, kwahiyo malumbano na chuki siku zote avijengi bali vinabomoa." alisema.

Pia mabeste amesema anachoangalia sasa ni kufanya kazi ambazo zitawafurahisha mashabiki zake na sio kuweka bifu na kinyongo na watu wengine.

'Ili Muziki wetu usonge mbele na ukue kama wa wenzetu, tunatakiwa kubadilika na kuiga mazuri kutoka kwa wenzetu, hivyo bado tuna safari ndefu sana ya kuufikisha huu muziki pale unapopaswa kufika." alisema Mabeste.

No comments:

Post a Comment