Thursday, June 16, 2016

BEN POL AWATAKA WASANII WENZAKE KUWEKEZA PESA KATIKA MUZIKI WAO ILI MUZIKI UWEZE KUFIKA MBALI

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amewataka wasanii wa muziki nchini kuwekeza pesa za kutosha kwenye muziki wao ili kuongeza thamani ya muziki wanaofanya.

Ben-Pol-2

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Moyo Mashine’ aliyoshoot Afrika Kusini, ameiambia Bongo5 kuwa uwekezaji kwenye muziki ndiyo siri ya kufanikiwa kwa wasanii wengi.
“Mimi nawaambia kwamba kama umeamua kuwa mmliki wa teksi au mmliki wa bajaji kumi au ishirini siyo mbaya ni biashara lakini kama umeamua kuwa mwanamuziki lazima uweke pesa kwenye muziki,” alisema Ben Pol.

Aliongeza, “Fanya shows ukipata milioni moja, chukua laki nane au tisa weka kwenye muziki, hiyo laki mbili fanya ndiyo profit. Ukipata milioni 10 chukua milioni 8 weka kwenye muziki na milioni mbili ndiyo faida tumia mpaka ambapo utaona hapa sasa navuna. Lakini wasanii wengi naona wapo katika hatua ya kuwekeza,”
Ben Pol amesema toka aanze kuwekeza pesa nyingi kwenye muziki wake, tayari ameanza kuona mabadiliko makubwa kwenye maisha yake ya muziki.

No comments:

Post a Comment