Saturday, June 11, 2016

KERI HILSON ATUA AFRIKA KWA SHINDANO LA AIRTEL TRACE MUSIC STAR

Tanzania inawakilishwa na Melisa John kwenye shindano la Airtel Trace Music Star linalokusanya vipaji vya Waimbaji Afrika, kuchuja na kumpata mmoja ambapo mwaka jana mshindi alikua ni Mtanzania Nalimi Mayunga ambaye tayari ameshafanya wimbo na Akon.

k6

Jaji mkuu wa mwaka huu ni mwandishi wa nyimbo na mwimbaji maarufu Keri Hilson kutoka Marekani ambaye tayari ameshawasili Nigeria kutazama vipaji vya vijana wa Afrika kutoka nchi 9 ikiwemo na Tanzania na kuisimamia fainali ya mwaka huu.

‘Naamini finali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki na kushuhudia vipaji vya kutosha, makuu tutakayoangalia wakati wa fainali ni pamoja na uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani jukwaani, uwezo wa sauti yake, naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto na nimejiandaa kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”

 

No comments:

Post a Comment