Friday, June 10, 2016

RAMA DEE ASEMA HAKUNA HAJA YA KUSHOOT VIDEO NJE WAKATI BONGO TUNA KILA KITU

Msanii wa muziki wa R&B wa Tanzania, Rama Dee anashangaa jinsi wasanii wa muziki wa Tanzania wanavyokwenda nje kushoot video za muziki wakati ndani wana kila kitu.

 http://tizneez.com/wp-content/uploads/2016/01/Rama-3.jpg

Muimbaji huyo ambaye aliachia wimbo ‘Kipenda Roho’ ambao unafanya vizuri, ameiambia BBC kuwa haoni kama ni sahihi wasanii wa ndani kwenda kufanya video zao za muziki Afrika Kusini.

“Hapa hapa kwetu kuna watu wanaweza kutengeza video nzuri bila shaka,” alisema Rama Dee. “Mimi huwa siamini issue ya Afrika Kusini au wapi, mimi naamini ukiwa na idea nzuri, kamera nzuri na unaweza kushare idea na director, munaweza kufanya kitu kizuri sana,”
Rama Dee yupu nchini Tanzania kimapumziko, kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake nchini Australia.

No comments:

Post a Comment