Thursday, June 16, 2016

WIZ KID NA TINIE TEMPAH KUSHOOT VIDEO VENEZUELA.

Muimbaji kutoka nchini Nigeria, Wizkid ameungana na Tinie Tempah rapper wa Uingereza nchini Venezuela kufanya video ya wimbo wao mpya.

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/06/x11821164_1639903142954587_408394810_n-2-300x194.jpg.pagespeed.ic.5pKnHYmbkk.jpg

 Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wizkid amepost picha akionekana wapo location nchini Venezuela akiwa na Tinie Tempah mwenye asili ya Nigeria. Hakuna shaka kuwa wawili hao kuonekana maeneo hayo hakuna kingine walichokifuata zaidi ya kushoot video.

Nyota ya Wizkid imeonekana kung’aa kwa mwaka huu kutokana na kuwa karibu na mastaa wakubwa duniani akiwemo Drake na Chris Brown huku wimbo wake na Drake ‘One Dance’ ukishikilia namba moja kwenye chati za Billboard 100 wiki sita sasa. 

353E824400000578-0-image-a-247_1465874484665

No comments:

Post a Comment