Monday, October 20, 2014

ALICHOKISEMA FA KUHUSU FIESTA 2014.

Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ni miongoni mwa wasanii waliopata nafasi ya kupanda jukwaa moja na rapper T.I kutoka Marekani, usiku wa Jumamosi October 18 pale viwanja vya Leaders Club jijini Dar katika tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2014.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTWOUfMXFyBTodtA8mmA2bF74-9aO83vCoHr_vojWkIZpRHOhpdBg_0b1hpLFiTj1jlDgIo0YY4zFR1RB1RR2DlAIKcZTHH_1cW8Ts14loocSje01yYbQs307nnOVDjLUuaaYZhWjppW1q/s1600/mwanafa_binamu.jpg
Mwana FA.
Licha ya kufanya show kali lakini pia Binamu alikuwa ni mtazamaji wa show za wasanii wengine wa Bongo na wale kutoka Nigeria, Kenya pamoja na mkali Clifford Joseph Harris a.k.a T.I.
Hiki ndicho alikiandika FA Instagram siku iliyofata baada ya show ya Fiesta:

"Nimeamini wabongo wanasupport na wanapenda muziki wao, hii imetokea baada ya kuona shangwe jana katka show ya Serengeti Fiesta! Nawapenda sana! keep supporting us!"

Show ilianza mapema mida ya saa 2:00 usiku na kufunguliwa na wasanii Chege na Temba kutoka Tmk, baada ya hapo walifata wasanii wengine na shangwe kuendelea kuwa kubwa baada ya kupanda TI ambaye wengi walikua wakimsubiri kwa hamu. kwa kifupi hivyo ndio mambo yalivyokua katika Serengeti Fiesta mwaka huu.



No comments:

Post a Comment