Wasanii wa hiphop wanaunda sehemu kubwa na ya muhimu katika muziki wa
Tanzania. Japo kuna watu wanaoamini kuwa ushindani kati ya rappers wa
Tanzania umepungua ukilinganisha na wasanii wa kuimba, bado tumeshuhudia
ngoma nyingi na kali zimetoka hadi wiki ya kwanza ya mwezi October
2014. Hawa ni wasanii 20 wa hip hop Tanzania waliosikika zaidi kwenye
redio, kuonekana zaidi kwenye TV, kufanya show nyingi ama nyimbo zao
kusikilizwa, kutazamwa na kuongelewa zaidi mtandaoni katika robo tatu ya
mwaka huu.
1. Joh Makini
Hakuna ubishi kuwa mwaka 2014 ulitawaliwa na Weusi. Kundi/kampuni hii kutoka Arusha imekuwa ikifanya kazi na kuachia jiwe baada ya jiwe bila kupumzika. Hata hivyo kazi kubwa zaidi imefanywa na mwamba wa kaskazini ambaye mwaka huu amekuwa rapper pekee kutoka Tanzania kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa. Pamoja na kufanya vizuri na anthem za Weusi, ‘Gere’ iliyoshuhudia wasanii hao wakisafiri hadi Kenya kwenda kushoot video yake pamoja na video ya ‘Nje ya Box’ iliyokuwa video yao ya kwanza kuwahi kuchezwa Channel O, Joh amefanya vizuri mwaka huu na wimbo wake ‘I See Me’ ambao video yake iliyoongozwa na Mkenya Enos Olik, itatoka hivi karibuni.

Joh ameendelea kuwa msanii wa hip hop anayetafutwa zaidi kwa collabo kwa sasa akiwa ameshirikishwa kwenye msululu wa hits za mwaka huu ikiwemo ‘Unanichora’ ya Ben Pol, ‘Ni Penzi’ ya Damian Soul, ngoma ya Belle 9 iliyotoka hivi karibuni ‘Vitamin Music’ na zingine. Upande wa show, ukimtoa Nay wa Mitego, hakuna msanii wa hip hop aliyepiga show nyingi kama huyu jamaa.
2. Mwana FA
Ilimchukua Mwana FA muda kiasi baada ya kutoa ‘Kama Zamani’, kuachia ngoma nyingine ya peke yake. Akiwa na ngoma nyingi kibindoni, alizorekodi kitambo na mpya, FA alijikuta njia panda kuchagua kutoa kati ya wimbo aliomshirikisha Alikiba na kutayarishwa na Marco Chali au ‘Mfalme’ aliyomshirikisha G-Nako na kupikwa na Nahreel. Bahati iliiangukia ‘Mfalme’ ambayo ilikuja kumuongezea orodha ya hits zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye vituo vingi vya redio.

Baada ya video ya wimbo wake na AY ‘Bila Kukunja Goti’, FA hajaonekana tena kwenye video mpya. Ni video ya ‘Mfalme’ aliyofanya na Mkenya Kevin Bosco Junior ndio itakuja kukata kiu ya mashabiki wake wanaomngoja kumuona tena kwenye video mpya.
3. Young Killer
Mr Blue anakiri kuwa uwezo wa Young Killer kiuandishi ni hatari kuliko umri wake. Ni kweli, rapper huyo wa Mwanza ameendelea kupata salute si tu kutoka kwa mashabiki wake, bali pia kwa rappers wakongwe wanaoheshimika.

Mwaka 2014, dogo huyu ameendelea kuuza ujuzi wake redioni kwa ngoma zake ‘My Power’ iliyo na video yake tayari na ‘Umebadilika’ ambayo alimshirikisha Banana Zorro. Video ya wimbo huo imeshafanyika na ipo kwenye maandalizi ya mwisho, chini ya muongozaji Hefemi. Katika kuashiria kuwa miezi miwili ya mwaka 2014 itabakia kuwa mizuri kwake, rapper huyo ameingia location kushoot video ya hit ijayo ‘13’ aliyomshirikisha kaka yake kimuziki, Fareed Kubanda aka Fid Q na muongozaji akiwa Nisher.
Tazama na soma waliobakia kwa kucklick HAPA

No comments:
Post a Comment