Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, YP amefariki dunia usiku wa
jana katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na
ugonjwa wa kifua.
Kiongozi wa kundi hilo Said Fela,
amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunamsubirika kaka yake kwa sababu YP kafariki usiku hospitali, Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo kafariki. Wazazi wa marehemu wapo Keko, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”
Taarifa zingine za kuhusu msiba wa mwanamuziki huyu zitatoka pale punde ndugu zake wakikaa na kuamua mazishi lini na taratibu zingine ni zipi.
![]() |
YP (KULIA) |

No comments:
Post a Comment