Taasisi
ya sanaa na utamaduni bagamoyo inatarajia kufanya Tamasha kubwa ambalo litakuwa
ni Tamasha la 34 tangu taasisi hiyo kuanzishwa, tamasha ambalo litafanyika katika
Kumbi na viunga vya Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo.
Wanafunzi wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. |
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Tamasha hilo John Mponda amesema
Tamasha litafanyika tarehe 21 hadi 27 na litahudhuriwa na watu kutoka nchi
mbalimbali lengo na madhumuni ni kuwapa fursa wanafunzi kuonyesha kile
walichojifunza kutoka chuoni hapo.
Aidha,
Mponda amesema tamasha hilo ambalo kauli mbiu yake ni SANAA NA UTAMADUNI KATIKA
UCHAGUZI HURU NA AMANI, kauli mbiu ambayo inahakisi uchaguzi Mkuu hapa nchini
hivyo kuwakumbusha watanzania na wao hawako nyuma kuitakia nchi amani na
utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi.
No comments:
Post a Comment