Monday, October 20, 2014

NILICHOKIONA NDANI YA SERENGETI FIESTA MWAKA HUU.

Fiesta ni Tamasha kubwa sana ndani na nje ya nchi hii , na wengi wakisikia Fiesta wanafahamu ni kitu gani kinakuja au kinafanyika, kutokana na tamasha hili kuwa maarufu sana imefkia hatua linalinganishwa na sikukuu kama Christmass na sikukuu zingine kubwa kimataifa.

 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/08/fiesta20141.png

Kuna baadhi ya mambo mimi kama mdau, mfatiliaji au mwandishi binafsi nimeyaona katika Serengeti Fiesta mwaka huu.

Cha kwanza ni Ratiba jinsi ilivyopangwa, Sikuelewa kwamba wasanii walitakiwa kuanza kuperform nyimbo zao kali zile zinazofanya vizuri mtaani au laa, manake kila msanii aliyepanda stejini alianza na wimbo wake ambao ndio uko hit yaani mkali. Tumezoea kuona kipindi cha nyuma kuwa msanii anapanda anafanya show then mwishoni ndo anamaliza na wimbo wake ambao anajua kwamba utaamsha mashabiki na kuwaacha wakiwa na hamu bado ya kupata burudani kutoka kwa msanii husika.

Cha pili ni Wasanii kadhaa ambao walishirikiana, i mean (Colable), Hii ilileta mkanganyiko pale ambapo baadhi ya wasanii walikuwa hawaendi kutoa support kwa mwenzie au kuimba ile verse ambayo ameshirikishwa na msanii huyo, sijui kama ilikua ni procedure but mimi kwa upande wangu sikuelewa nini kilichokua kinaemdelea manake ilifika hatua mpaka msanii anamuita msanii mwenzie lakini cha ajabu msanii anayeitwa atokei stejini, inashangaza kwa Tamasha kubwa ambalo linaaminika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wake kufanya mkanganyiko wa namna hii, aya ni maoni yangu tu.

Cha tatu ni misunderstanding za wasanii husika, hili liko nje kabisa ya uwezo wangu but ntalizungumzia kidogo, kuna muda alipanda Diamond Platnumz kufanya show yake lakini cha ajabu alizomewa sana na alipapanda Ali Kiba shangwe zikawa nyingi sana, kuna mambo mengi yanazungumzwa mitaani kwa sasa kuwa kuna mambo yanafanywa na watu ili kumuona msanii fulani hawezi, kama utakuwa shahidi Fiesta ya mwaka jana kitu kama hiki kilitokea kwa msanii huyu huyu (Diamond), baaada ya siku kadhaa kundi la watu fulani lilisema walipewa pesa kumzomea, sasa muziki wetu unaenda wapi? unakuwa au unapotea? unafanya vizuri au tunauaribu wenyewe? haya ni baadhi tu ya maswali niliyokuwa najiuliza bila kupata majibu.

Hii sio nzuri TUBADILIKE, tupende vya kwetu! kuzomeana na kupigana majungu hivi vitu vimepitwa na wakati. Haya yalikuwa ni maoni yangu kwa nilichokiona katika Serengeti Fiesta Mwaka huu. Ni matumaini yangu next year watarekebisha makosa yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment