Monday, October 6, 2014

ONE THE INCREDIBLE KUACHIA MIXTAPE YA NGOMA 100.

Msanii wa Hip Hop, One The Incredible anatarajia kuachia mixtape yenye nyimbo 100… Yes nyimbo mia moja, pamoja na album yenye ngoma 22. Ngoma hizo zipo kwenye hatua ya mwisho (pengine ndio maana alikuwa kimya.
http://voturadio.com/wp-content/uploads/2012/05/One-the-incredible.jpg
ONE THE INCREDIBLE.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa amezunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kukamilisha mixtape na album hiyo.
“Yeah kuna mixtape yangu inakuja lakini sasa hivi nipo kwenye maandalizi ya kumalizia kwanza album yangu ya nyimbo 22, ikishamalizika ndo naanza kumaliziamalizia mixtape yangu ya nyimbo 100,” amesema. “Kwenye hii mixtape nipo pia kwenye maandalizi ya mwisho. Nimezungumka kwenye mikoa mbalimbali Tanzania nzima ili kukamilisha mixtape, kwahiyo hii mixtape itakuwa na wasanii mbalimbali kutoka mikoani,” ameongeza.
One amezungumia pia kujipanga na soko na album na njia atakazotumia kuweza kuuza album hiyo.
“Ingawa soko haliko poa sana ila kuna njia mbili nimezipata ili kuwafikia watu wangu. Kwanza nitauza kwa njia ya mtandao kama kawaida yangu, watumiaji wa mitandao kwa sasa ni wengi sana kwahiyo nitauza hivyo hivyo. Pia nitafanya tour mbalimbali za kuweza kufanya niuze, kwaiyo nitafanya uzinduzi wa album nipo kwenye maandalizi ya ukumbi nitapata mtasikia tu.” (Story kwa msaada wa Bongo 5.)

No comments:

Post a Comment