Kundi linalofanya vizuri kwa sasa katika muziki wa Hip Hop tanzania, Weusi linatarajia kuanza show yao ya funga mwaka ambayo wanaifanyaga kila mwisho wa mwaka, kundi hili ambalo pia ni kampuni inayojishughulisha na kuprint T shirts zao za aina tofauti tofauti zenye logo ya Nyeusi linatarajia kuanza show hiyo siku ya tarehe 1 Jijini Arusha katika ukumbi wa Triple A.
Wapo wasanii wengine ambao watawasindikiza tamasha hilo akiwemo Ben Pol, Vanessa Mdee, Jambo Squad na wengine wengi tu, hii ni desturi ya Weusi kufanya show ya kufunga mwaka kila inapofika mwisho wa mwaka kuwapa burudani mashabiki zao na kuukaribisha mwaka mpya kwa ajili ya kujipanga kwa kazi zingine za kimuziki.
Vilevile Bonta atakuwa anaachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la B3 aliyomshirikisha G Warawara ambayo imefanywa na Q the Don pamoja na Chizan Brain, na ngoma hiyo itakwenda kuskika kwa mara ya kwanza katika tour hiyo ya Funga mwaka.
Haitaishia Triple A, bali tarehe 8 itakuwa ni zamu ya Moshi kupata burudani na Weusi, coz moshi na Arusha ndio nyumbani kwahiyo haina budi show kuanzia pande zile. Baada ya hapo taratibu za kuendelea na mikoa mingine zitaendelea. Funga mwaka na hawa jamaa!!!!!!!
![]() |
WEUSI. |

No comments:
Post a Comment