Saturday, May 28, 2016

MWIMBAJI WA MUZIKI WA DANSI KHALID CHOKORAA RASMI KAONDOKA MAPACHA WATATU




Mwimbaji wa muziki wa Bendi Khalid Chokoraa ni miongoni mwa wakali wenye majina yao kwenye muziki wa dansi, alipata time ya kuzungumza na kituo kimoja cha Online Tv na akazungumzia taarifa za yeye kutoka bendi ya Mapacha Watatu na kwenda Twanga Pepeta……

http://www.bongossip.com/wp-content/uploads/2014/10/904achokoraa.jpg
Khalid Chokoraa.
 nimeamua kuondoka bendi ya mapacha watatu, lakini kiheri kabisa, hakuna tatizo wala bifu kikubwa zaidi ni maisha tu, kilichoweza kunisukuma nilijiuliza tunafanya kazi ili tuwe na maisha mazuri ndani ya miaka minane nimefanya nini mbona naona kama siendi vile imetokea mtu ameweka mzigo nikaona tunafanya kazi ili tunatafuta pesa na pesa imekuja’

‘Twanga nilikaa pale miaka mitano nikafanya album nne niliacha viporo vya kazi zangu nyingi sana kwa hiyo nikirudi sitaumiza kichwa sana kwa sababu mashabiki wa muziki wa dansi wanajua nini nilikifanya ndani ya Twanga Pepeta’;-Khalid Chokoraa

‘Nimepewa ada ya kunirudisha namshukuru Mwenyezi Mungu siwezi kusema ni ndogo au ni nyingi lakini kwa usawa huu wa Magufuli wa kutumbua majipu ni nyingi, kwa kibendi bendi inawezekana katika wanamuziki wa bendi mimi nikawa ni mwanamuziki niliyenunuliwa kwa bei kubwa’:-Khalid Chokoraa.
Kuazaa video ya mahojiano ya Khalid Chokoraa Click HAPA

No comments:

Post a Comment