Kesi
iliyokuwa inamkabili staa kutoka Marekani Chriss Brown juu ya malezi
mabovu ya mtoto wake ambayo ilifunguliwa na mzazi mwenzake Nia Guzman,
May 24 maamuzi yalitolewa na Mahakama ya Califonia.

Mama mtoto
wa Royalty alidai kuwa Chris hana malezi sahihi na muongozo unaostahili
juu ya mtoto wao, amesema Chris amekuwa akivuta sigara na bangi yeye na
marafiki zake mbele ya mtoto wao na imempelekea Royalty kupata maradhi
ya pumu.
Nia Guzman aliomba
mahakama impunguzie Chris muda wa malezi ya mtoto huyo na kuomba yeye
ndiye achukue jukumu la usimamizi wa mtoto wao kwa kipindi hiki. Chriss
Brown ameshinda kesi hiyo ambapo maamuzi ya jaji yaliruhusu malezi sawa
kutoka kwa wawili hao ambapo Chriss anaruhusiwa kuspend siku 12 na mtoto
wake kila mwezi bila masharti yoyote.
No comments:
Post a Comment