Friday, June 24, 2016

RAPPER KUTOKA SOUTH AFRICA CASPER NYOVEST AWA ARTIST WA KWANZA KUTOKA SOUTH AFRICA KUFANYA INTERVIE KATKA KIPINDI CHA SWAY IN THE MORNING... NDANI STATION KUBWA TOKA MAREKANI.

Rapper Cassper Nyovest amekuwa msanii wa kwanza wa Afrika Kusini kuhojiwa kwenye kipindi maarufu cha redio nchini Marekani, Sway in The Morning.

13473093_1856705074462521_355726459_n

Kwenye show hiyo Sway alimuuliza rapper huyo masuala mengi kuhusiana na muziki wa hip hop wa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla. Lakini mambo yalikuja kunoga zaidi baada ya mtanzania aitwaye Emmanuel alipopiga simu.

“We got the whole continent down here,” alisema Sway baada ya Emmanuel kusema kuwa anapiga simu kutoka Tanzania.

Cassper alichombeza kwa kusema, “Diamond’s land.” Swali ni je, alimaanisha Diamond Platnumz au madini ya almasi? Kuna uwezekano akawa amemaanisha Chibu hasa kwasababu wote mwaka huu wanawania kipengele cha Best African Act: Africa kwenye tuzo za BET zitakazotolewa Jumamosi hii.

Kusikiliza interview ya Casper BOFYA HAPA.

No comments:

Post a Comment