June 2,
2016 label ya Wasafi inayomilikiwa na staa Diamond Platnumz inaingia
kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi msanii
wao mpya Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa
kazi zake katika label hiyo.
Kwa mujibu wa Diamond Platnumz amesema…’
Kwasasa
Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii wanne ukiachana na Rich Mavoko
kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini
anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa
na Raymond, Harmonize, Rich Mavoko na Queen Darling’
![]() |
Rich mavoko na Diamond Platnumz. |
Baadhi ya watu wameanza kuzungumza kuwa Rich Mavoko ni msanii mkubwa hivyo kusaini WCB ni kujishuasha, ila ningependa kuwakumbusha kuwa Kanye West ni Msanii mkubwa duniani lakini alisaini lebel ya Jay Z ya Rock Nation.
Kwahiyo sioni tatizo kwa Rich mavoko kuwa chini ya lebel ya WCB, kinachotalkiwa ni maslahi yake yaende kama walivyokubaliana.
Kutazama video ya utambulisho wake CLICK HAPA
No comments:
Post a Comment