Monday, July 18, 2016

NAY AITWA BASATA, NI JUU YA WIMBO WAKE "PALE KATI"

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limemwita msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ikiwa ni siku chache toka watangaze kuufungia wimbo wake ‘Pale Kati’ kutokana na wimbo huo kudaiwa kukiuka maadili.

Nay true boy

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema kwa sasa hawezi kulizungumzia swala la kufungiwa kwa wimbo wake mpaka pale atakapofanya kikao na BASATA.

Nay wa Mitego

“Kesho nimeitwa BASATA, nadhani itakuwa ni vizuri nikizungumzanao, alafu ndo nije kuzungumza issue ya kufungiwa,” alisema Nay.

Hapo awali rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ utakuwa na video nne tofauti tofauti ambapo mpaka sasa tayari ameshashoot video mbili, moja akiwa ameshoot Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment