Ligi Kuu England kwa
kushirikiana na chama cha soka cha nchi hiyo leo July 20 2016
kimetangaza sheria mpya kwa ajili ya kuwalinda marefa na wachezaji
wanaoonesha vitendo vya utovu wa nidhamu mbele ya waamuzi au kuonesha
ishara na vitendo vya kupinga maamuzi yao.

Taarifa iliyotolewa na tovuti rasmi ya Ligi Kuu inasomeka
“Mamlaka za soka England zimegundua kukithiri kwa vitendo vya utovu wa
nidhamu kwa wachezaji na makocha wa Ligi Kuu kwa misimu minne iliyopita,
kwa sasa vitendo hivyo vimefikia katika hatua ambayo haiwezi kuzoeleka”
Sheria hii itakuwa inahusu au
imemuongezea muamuzi mamlaka ya kuonesha kadi ya njano au nyekundu kwa
vitendo ambavyo awali vilikuwa vinaachwa kama kumfuata kwa reaction
kubwa muamuzi kutokana na kutokubali maamuzi fulani, hata hivyo Wayne Rooney na Diego Costa huenda watakuwa waathirika wakubwa wa sheria hii.

MCHEZAJI ANAWEZA ONESHWA KADI YA NJANO KWA KUFANYA YAFUATAYO
- Kuonesha kitendo cha kukosa heshima kwa wasimamizi wa mechi
- Kuonesha vitendo au dalili za kupinga maamuzi ya refa
- Kumfuata refa au msaidizi wake na kuzozana uso kwa uso
- Kumkimbilia au kumfuata muamuzi kwa jazba na kupinga maamuzi yake
- Kutoa matusi au lugha chafu inaweza kumuweka mchezaji hatiani
- Kugusa au kumfuata muamuzi na kusukumana nae kwa kifua kama mchezaji mwenzako
- Refa anaruhusiwa kumuonesha kadi ya njano mchezaji kinara wa kuongoza kumzonga refa au msaidizi wake.
- Mchezaji anaweza oneshwa kadi nyekundu kwa kumzonga, kumtukana refa au kumtusi kwa lugha ya ishara.
- Kuzongana au kumpiga kikumbo muamuzi kutokana na kutoridhishwa na maamuzi yake.
No comments:
Post a Comment