Monday, August 22, 2016

LE BRON JAMES NA STEPHEN CURRY WAIPONGEZA TIMU YA KIKAPU YA MAREKANI KWA KUSHINDA MEDALI YA DHAHABU.

Mastaa wa kikapu LeBron James na Stephen Curry wameipongeza timu ya taifa ya kikapu ya Marekani kwa kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki huko Brazil yaliyofungwa jana.

Baily

Timu hiyo ya Marekani iliyokuwa ikiongozwa na mchezaji Kevin Durant chini ya kocha mkuu wa timu hiyo
Mike Krzyzewski ilifanikiwa kushinda medali hiyo kwenye mchezo wake wa fainali baada ya kuifunga timu ya kikapu ya Serbia kwa jumla ya vikapu 96 dhidi ya 66.

Baada ya mchezo huo LeBron James aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter, “S/O #USABMNT on nearing their🏅!! #GoldStandard #USA #StriveForGreatness.”
“Congrats 2 @usabasketball taking care of business & getting the Gold! Go down the line, they all put in the sacrifice & work 2 get it done!,” ameandika Stephen Curry kwenye mtandao huo.

Marekani ndiyo iliyofanikiwa kuchukuwa medali nyingi kwenye mashindano hayo ikiwa imejikusanyia jumla ya medali 121 ikifuatiwa na China iliyopata jumla ya medali 67.

No comments:

Post a Comment