Monday, September 5, 2016

VANESSA MDEE ATUMBUIZA NA 2 FACE IDIBIA KWENYE SHOW YA BUCKWYLD N BREATHLESS, LAGOS.

Katika sehemu ambayo Vanessa Mdee ameshalikita jina lake vyema nje ya Tanzania, basi ni Nigeria.

14052650_265827230482621_1149670948_n

Muimbaji huyo wa ‘Niroge’ Jumamosi hii alikuwa mmoja wa waimbaji walioipamba show kubwa ya msanii mkongwe wa Nigeria, 2 Face Idibia iliyopewa jina, Buckwyld N Breathless. Show hiyo ilifanyika Eko Hotels & Suites, jijini Lagos.

14135101_1751452555138222_1959659388_n

Vee ambaye alitengeneza pair iliyovuma zaidi kwenye Coke Studio Afrika mwaka jana na 2 Face, hakuwa mchoyo wa fadhila kumshukuru muimbaji huyo kwa nafasi aliyompa.
“This picture describes everything I was feeling last night,” ameandika Vanessa kwenye picha akiwa na 2 Face jukwaani aliyoiweka Instagram.

“I thankyou @official2baba for constantly inspiring and elevating youngns like myself. I’m humbled and eternally gratefully.”

2 Face amewahi kukaririwa akimtaja Vanessa kuwa ni mmoja wa waimbaji anaowakubali Afrika.

No comments:

Post a Comment