Thursday, September 25, 2014

PROFESSOR J: WANIGERIA WAUA MZIKI WETU, WATUPELEKA WANAVYOTAKA.

 Professor Jay amedai kuwa wasanii wa Nigeria kwa kiasi kikubwa wamewatawala wasanii wa Tanzania na wanawapeleka vyovyote watakavyo.
 
http://nairobiwire.com/wp-content/uploads/2014/03/prof-j.jpg
PROFESSOR J.
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM hivi karibuni, Professor alisema wasanii wengi wa Tanzania wamekosa ubunifu wao wenyewe na wamekuwa wakiiga mambo mengi kutoka Nigeria. “Hakuna mtu anakuja na idea ya kufanya kitu tofauti, ukija na idea moja tu ikaonekana imefanya vizuri watu wote wanahamia huko,” alisema Professor.

Professor alidai muziki wa Nigeria hauna miaka mingi ukilinganisha na ule wa Tanzania lakini hivi sasa umefika mbali kiasi cha kuutawala muziki wa Afrika.

“Najisikia aibu kusikia nipo zaidi ya miaka 20 kwenye game halafu bado napiga mark time ni jinsi gani nitakamata hata soko la Rwanda tu, ni aibu.” Alisema.

 Hii ni aibu kubwa sana kwa mziki wetu, kinachotakiwa ni kufanya mziki wa Tanzania uende International kama watu wa Nigeria wanafanya kwao, na hii haiji hivihivi bali kwa kupeana support ya kutosha.

No comments:

Post a Comment