Jarida la Forbes limetoa orodha yake ya wasanii wa Hip Hop wanaolipwa
fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka huu, ‘The 2014 Hip-Hop Cash Kings’
na Dr Dre amekamata nafasi ya kwanza kwa mara nyingine.
 |
DR. DRE. |
Dre Dre amepewa ufalme huo kwa kutengeneza $620 million kupitia
biashara zake, na kumfanya arudi kwenye nafasi ya kwanza aliyoikamata
mwaka 2012 kabla ya kuenguliwa na Diddy mwaka jana huku yeye akijikuta
kwenye nafasi ya tatu.
Pamoja na kwamba Dre hajatoa album wala kufanya tour yoyote kwa miezi
12 iliyopita, lakini dili la Apple kuinunua kampuni yake ya Beats
Electronics kwa $3 billion ndio imemfanya atengeneze fedha nyingi zaidi.
 |
JAY Z & DIDDY. |
Jay Z na P Diddy wamefungana kwenye nafasi ya pili kwa kutengeneza $60 million kila mmoja.
 |
DRAKE. |
Nafasi inayofata imekamatwa na Drake kwa kutengeneza $33 million, zilizotokana na album yake ya "Nothing was the same" endorsment deal yake, Nike pamoja na Tour. Tazama orodha ya wanaowafatia hawa Jamaa kwa kuclick
HAPA.
No comments:
Post a Comment