Monday, October 27, 2014

NIKKI MINAJ KUACHIA NGOMA MPYA.

Ikiwa ni mwezi mmoja umebaki kabla hajaachia album yake ya tatu ‘The Pinkprint’, na miezi miwili toka aachie single ya ’Anaconda’, Nicki Minaj kesho Jumanne (Oct. 28) anatarajia kuachia single mpya iitwayo ‘Only’.
Only
Katika single hiyo Minaj amewakutanisha Drake na Chris Brown pamoja na Lil Wayne.
Minaj ameshare cover ya kuchorwa ya single hiyo ambayo inamuonesha Drizzy akiwa amevaa kama papa bila uwepo wa Breezy.
Album ya Nicki Minaj ‘The Pinkprint’ inatarajiwa kutoka November 24 chini ya Young Money, Cash Money na Republic Records.

No comments:

Post a Comment