Wednesday, June 22, 2016

DOGO KUTOKA GHANA APATA SHAVU LA KUIGIZA MOVIE YA SPIDER MAN.

Jina lake kamili ni Abraham Attah na umri wake ni miaka 25 tu, umaarufu wake ulikuwa mkubwa baada ya kuonekana kwenye movie ya Beasts Of No Nation ambayo ndani aliigiza pia mwigizaji maarufu wa Marekani Idris Elba.



Attah kwenye kazi ya uigizaji pamoja na Idris Elba, kipaji cha mtoto huyu wa Ghana kiligunduliwa na Muongozaji wa filamu wakati wa mechi moja ya mpira wa miguu huko Ghana.

Attah


Movie mpya atakayoonekana Attah ni Spider-Man: Homecoming ambayo inaanza kutengenezwa muda wowote kuanzia sasa na itayafikia majumba ya Cinema July 2 2017 ndani yake kukiwa na mastaa kama Hannibal Buress, Logan Marshall-Green, Donald Glover, Zendaya and Tony Revolori.
Unaweza kumtazama Attah alichofanya kwenye BEASTS OF NO NATION kwenye hii Trailer hapa chini akicheza kama Mwanajeshi mtoto. BOFYA HAPA kutazama Trailer ya movie hiyo aliocheza Abraham Attah

No comments:

Post a Comment