Thursday, June 30, 2016

JENNIFER HUDSON ASAINI MKATABA NA EPIC RECORDS.

Msanii wa kuimba na mwigizaji maarufu kutoka Marekani, Jennifer Hudson amesaini mkataba na kampuni mpya ya Epic Records.

chemical-kama-ipo

Kabla ya kusaini mkataba na lebo ya Epic Records, Hudson aliwahi kuwa chini ya lebo kadhaa zikiwemo Arista Records, J Records na RCA Records.

Baada ya kumsaini mkataba mpya na Epic Records, Hudson kupitia akaunti yake ya instagram aliandika, “I have no doubt in my mind , this is going to be EPIC! #epicrecords.” Nao kampuni ya Epic Records kupitia akaunti yao ya twetter waliandika: “We are THRILLED to welcome @IAMJHUD to the EPIC family!👏💖✨New 🎶🎶 coming soon – woot woot! #BeEpic”

Mpaka sasa kampuni ya Epic Records inawasimamia mastaa kadhaa wakubwa akiwemo Jennifer Lopez, Mariah Carey, Fifth Harmony na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment