Shambulio la bunduki na bomu kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Ataturk uliopo kwenye mji mkuu wa Uturuki, Istanbul limesababisha vifo
vya watu 36 na kuwaacha wengine zaidi 140 wakiwa majeruhi.
Washambuliaji watatu walianza kushambulia kwa bunduki nje na ndani ya uwanja huo wa ndege usiku wa Jumanne hii na walijipua kwa bomu baada ya kushambuliwa na polisi. Waziri Mkuu, Binali Yildirim amesema kuwa dalili za mwanzo zinaonesha kuwa kundi la Islamic State limehusika na shambulio hilo.
Picha kutoka kwenye uwanja huo wa ndege zimeonesha miili iliyofunikwa na mashuka huku vioo na mizigo ikiwa imesambaa kwenye jengo hilo.
Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan amesema shambulio hilo litumike kwa dunia kuwekeza nguvu kubwa katika kupambana na makundi ya wanamgambo. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.

No comments:
Post a Comment