Wednesday, June 22, 2016

Mr. T TOUCH ASEMA SIO LAZIMA KUANIKA MAFANIKIO YAKO KAMA NI STAA

Mtayarishaji wa muziki Bongo anayefanya vizuri kwa sasa, Mr T-touch ameeleza sababu ya kutokuonekana kwa mafanikio yake kwenye maisha japo amekuwa ni producer mkubwa kwa sasa.

Prezzo-vs-Jaguar

Akiongea na kipindi cha Clouds E, kinachoruka kupitia Clouds TV, T-touch alisema, “Siyo producers tu kuna baadhi ya wasanii wengine ni wasanii wakubwa maisha yao na wanachokipata havilingani.

“Kwahiyo siwezi kusema mimi ni mimi tu na mtu mwengine hawezi kujua nafanya nini, kunamafanikio ambayo yako wazi na kuna mafanikio ambayo hayapo wazi,” aliongeza.

Mr T-touch aliendelea kwa kusema, “Mimi siyo kama msanii nifanye kitu kuwaonyesha watu, labda nina mjengo huko lakini mtu hajui. Mtu mwengine akikuona anajua Mr T si yupo tu, kwaio mtu akinijaji simshangai kutokana na vile anavyoniona.”

No comments:

Post a Comment