Friday, June 3, 2016

PRINCE MUIMBAJI WA MAREKANI ALIFARIKI BAADA YA KUZIDISHA DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU

Muimbaji wa Marekani, Prince alifariki kutokana na kuzidisha kwa bahati mbaya dawa za kupunguza maumivu, Fentanyl, wachunguzi wa mwili wake wamesema.

image
Prince

Ripoti kutoka ofisi Midwest Medical Examiner ya jimbo la Minnesota, imekuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya muimbaji huyo kukutwa hajitambui kwenye lifti iliyopo kwenye nyumba yake.
Wapepelezi tayari wamemhoji daktari aliyemuona mara mbili muimbaji huyo aliyekuwa na miaka 57 wiki kadhaa kabla ya kifo chake.

Waranti ya polisi imeonesha kuwa Dr Michael
Schulenberg alimwandikia dawa hizo muimbaji huyo Aprili 20 – siku moja kabla hajafa.
Wanasema Fentanyl ni dawa yenye nguvu kuliko hata madawa ya kulevya aina ya heroin na hupewa zaidi wagonjwa wa saratani wenye maumivu makali.

Prince alipatikana hajitambui kwenye lifti za Paisley Park
Studios asubuhi ya April 21.
Alichomwa moto kwenye mazishi ya faragha April 24. Familia yake inapanga kuwa na shughuli za kuagwa na umma mwezi August.

No comments:

Post a Comment