Thursday, July 28, 2016

DAYNA NYANGE ATOA SABABU YA KUTOSHIRIKISHA WANAWAKE WENZIE KWENYE NGOMA ZAKE.

Wasanii wengi wa kike kwenye muziki hapa Bongo wamekuwa wagumu katika kushirikishana kwenye nyimbo zao, mmoja kati ya wasanii hao ni Dayna Nyange.

Dyna-Nyange
 
Akiongea na Bongo5, Dayna amesema kuwa kwa sasa ideas nyingi anazokuwa nazo zinahitaji sana wasanii wa kiume pekee.

“Siwezi kusema kuwa nawatenga wasanii wenzangu wa kike kufanya nao kazi, kila kitu kina wakati wake. Nitafanya nao kazi pale nitakapoona inahitajika nifanye nao kazi. Nashindwa kufanya nao kwa sasa kwa sababu idea nyingi ninazokuwa nazo zinahitaji wasanii wa kiume pekee,” amesema Dayna.

“Lakini nashukuru angalau nilishawahi kufanya kazi na Misoji Nkwabi aliyekuwa mshindi wa BSS,” ameongeza.

No comments:

Post a Comment