Thursday, July 28, 2016

KID BWAY ABARIKI SAFARI YA MAFANIKIO YA BARAKA DA PRINCE.

Producer na mtangazaji wa redio mkongwe, Sandu Mpanda aka Kidboy aliyemweka Barakah Da Prince kwenye ramani ya muziki kupitia Tetemesha Entertainment, ametoa maoni yake kuhusiana na uhamaji wa Barakah kwenda RockStar4000 na kusema ni njia nzuri kama atafikia malengo aliyojiwekea.

Kid Bway3

Akiongea na E-News ya EATV, Kid alisema, “Nitafurahi akifikia yale malengo niliyokuwa nayo kichwani wakati naanza kufanya naye kazi. Hata kama atayafikia kwenye njia tofauti na nilizoona mimi, nitafurahia kwa mafanikio yake kama ndio njia itakayomfikisha.”

1467189524_2976_b

“Muda mwingine unatakiwa kujitoa hata kama utaumiza watu ili ufanikiwe, siwezi kumtakia mabaya,sio vizuri kumuombea mtu vitu vibaya,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment