Tuesday, July 26, 2016

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU STAA WA BOLLYWOOD SALMAN KHAN.

Muigizaji wa filamu nchini India, Salman Khan, ameachiliwa huru na mahakama moja kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mnyama wa mwituni aliye katika hatari ya kuangamia kabisa duniani.

Indian Bollywood actor Salman Khan (2R) celebrates and wishes his fans Ramzan Eid Mubarak at his residence in Mumbai on July 18, 2015.  AFP PHOTO        (Photo credit should read STR/AFP/Getty Images)

Alikuwa ameshtakiwa kwa kuwaua swala watatu katika jimbo la Kaskazini la Rajasthan mwaka wa 1998. Mwaka uliopita aliachiliwa na mahakama kwa kosa jingine la kumkanyaga na kumuua mtu asiye na makazi.
Salman Khan, ni nyota wa filamu kutoka Bollywood, ambaye ana sifa ya kujikuta mashakani mara kwa mara. Mwaka 1998 alilaumiwa na kabila moja la Rajasthan kwa kupiga risasi na kuwaua swala watatu wakati alipokuwa katika shughuli za uwindaji.

Swala hao wanalindwa kisheria na pia wanasujudiwa na kabila lililoshtaki.
Alikuwa amepatikana na kosa na mahakama ya chini na kuhukumiwa kifungo lakini sasa ameachiliwa baada ya kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment