Saturday, April 29, 2017

Bondia Frances Miyeyusho kutinga ulingoni nchini Ujerumani

Bondia Mtanzania Frances Miyeyusho, amekwea pipa hapo jana kuelekea nchini Ujerumani kwa ajili ya Pambano lake lisilokuwa la Ubingwa dhidi ya Bondia kutoka nchini humo James Cheleji.



Mchezo huo utakaochezwa Aprili 29, katika jiji la Munich, Bondia huyo ameondoka nchini pamoja na Bondia Mkongwe, Emanuel Mlundwa katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.



Miyeyusho amewataka watanzania kumuombea ili aweze kufanya vyema katika pambano hilo, kumuwezesha kupata fursa ya mapambano mengi zaidi ya kimatafa na kuiwakilisha nchi katika medani za kimatifa kupitia mchezo huo wa Masumbwi.


No comments:

Post a Comment