Saturday, April 29, 2017

Fid Q: Sijawahi kujuta kumnyima Edu Boy namba yangu

Fid Q amefunguka baada ya kuchanwa na Edu Boy kwenye wimbo wa ‘Naiee’.



Katika wimbo huo ambao Edu amemshirikisha Bilnass, rapa huyo amemchana Fid kwa kusema, “Sio kwamba simpendi Fid Q, ila roho iliniuma aliponinyima namba.”

Akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, “Sijawahi kujuta kumnyima Edu Boy namba yangu, kwasababu namba yangu sio ya taifa. Kibaya zaidi sikua namfahamu kwa hiyo sidhani kama nilifanya makosa. Alichokifanya kuniimba kwenye ngoma yake sijaona kama kakosea, nahisi alikuwa anatafuta attention kwenye ngoma yake.”

Baadhi ya mastaa waliochanwa kwenye wimbo huo ni pamoja na Madee, Young Killer, Vanessa Mdee,Linex, Ben Pol na wengine.

No comments:

Post a Comment