Saturday, April 29, 2017

Lewis Hamilton: Mercedes wataingiza kikosi kazi ili kuishinda Ferrari.

Dereva mahiri wa Mercedes, Lewis Hamilton, amesema kuwa timu yao ya Mercedes itahakikisha inafanya kazi kwa pamoja ili kuwashinda mahasimu wao wakubwa ambao ni Ferrari. Hamilton amesema Ferrari ni mahasimu wao wakubwa na hivyo inatoa tafsiri ya kuwa ni lazima kuweka juhudi katika kuwashinda.



Tumaini kubwa ni kufanya kazi kwa Bahrain na huo utakuwa ni mthiani tosha katika mchezo huo, Hamilton anaamini madereva wa magari ya Mercedes’ watafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano zaidi kuwahi kutokea ili kuwashinda wapinzani wao wa Ferrari.

Hata hivyo dereva huyo mwenye jina kubwa katika mashindano ya Formula 1, anaamini wataibuka Mabingwa wa Dunia katika mashindano hayo ambayo watingia kwa mtindo wa kushambulia wapinzani wao katika mchezo wa Mwishoni mwa juma hili wa Russian GP baada ya kurekebisha makosa yao yaliojitokeza katika mchezo uliopita.

No comments:

Post a Comment