Wanandoa Isaac Vatkin (91) na mkewe Teresa (89) waliofunga ndoa miaka 69
iliyopita wameishangaza dunia baada ya kufariki wakiwa wameachana kwa
saa moja pekee.
 |
| ISAAC VATKIN NA TERESA. |
Wawili hao, ambao walikuwa wakiishi katika eneo la Illinois mjini
Chicago, walifariki Jumamosi iliyopita. Inadaiwa kuwa Teressa ndiye
alikuwa wa kwanza kufariki dunia kwa ugonjwa wa Alzheimers, ambapo wote
wawili walikuwa wakipata matibabu katika hospitali ya Highland Park
Hospital.
Wakati Teressa anafariki dunia, mumewe Vatkin alikuwa amemshika mkono
akiwa katika kitanda kilichokuwepo jirani na kile alicholala mkewe. Kwa
mujibu wa wauguzi katika hospitali hiyo, dakika 40 baadae Issac
alifariki dunia kwa tatizo la kushindwa kupumua vizuri.
 |
| WAKATI WA NDOA YAO MIAKA 69 ILIYOPITA. |
Clara Gesklin ambaye ni mtoto wa wazee hao, ameiambia Daily Mail,
“Upendo baina yao ulikuwa mkubwa sana, mmoja asingeweza kuishi bila
mwenzake.”
No comments:
Post a Comment