Monday, September 29, 2014

T.I.D ATAKA SUPPORT KATIKA GAME.

Muimbaji wa ‘Kiuno’, TID amesema tangu siku nyingi yeye ni msanii wa kimataifa ingawa amekuwa hapewi support anayostahili kupata.

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/08/TID-Khalid-Mohamed.jpg
TID.
  Akiongea kuhusu swala hilo, muimbaji huyo ambaye hivi karibuni alirekodi wimbo na msanii wa Afrika Kusini, Tumi, amesema kile wanachokifanya wasanii wapya wanaotaka kwenda international kwa sasa, yeye alikifanya miaka mingi iliyopita.
 “Unajua kama kufanya muziki international mimi tayari nilishaenda zamani sana, maana nikikumbuka video zangu nimeshafanya interviews na MTV Base,Channel O na pia nimefanya kazi na wasanii kutoka Nigeria na South Africa,” amesema.

“Pia nimefanya kazi na watu kama akina Chameleone na wasani wengine. Kwahiyo kwenda International ndo kitu nachokifanya. Naona ni support ndo sipati ya kutosha maana nimeshafanya maconcert makubwa kama Kigali,Burundi na South Africa kwahiyo muziki wangu upo international.”

No comments:

Post a Comment