Friday, September 26, 2014

YOUNG KILLER NA FID Q KUFANYA NGOMA PAMOJA!

Rapper kutoka Rock city Young killer Msodoki wiki hii amerekodi ngoma mpya ambayo amemshirikisha kaka yake Fareed Kubanda Fid Q, ambaye pia anatoka mwanza.
 
msodoki na fid2
YOUNG KILLER & FID Q.
 Msodoki amezungumza kuhusu wimbo huo, “Ni project mpya kabisa kali naweza kusema kwasababu imekutanisha wakali wawili halafu kutoka mji mmoja”, alisema Killer.
Amesema kuwa jina la wimbo huo ’13’, limetokana na tarehe ya kuzaliwa yeye na Fid ambao wanashare tarehe moja ya kuzaliwa lakini mwezi na mwaka tofauti.

“Hii ngoma inaitwa ‘Kumi na Tatu’ (13), kumi na tatu ni tarehe ila hatujaamua kuiita tarehe 13 ila inaitwa 13, kwasababu tarehe 13 ni siku ambayo kazaliwa Fid Q na ndio siku ambayo nimezaliwa mimi kwahiyo wote ni 13, kwahiyo ngoma tumeamua tuiite 13.”
Fid amezaliwa August 13 huku Msodoki April 13. Kusoma zaidi story hii ya hawa Ruppers Click hii LINK

No comments:

Post a Comment